Leo March 20, 2018 ni Siku ya Furaha Duniani. Siku chache tu zilizopita Umoja wa Mataifa walitoa ripoti ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na furaha na huzuni duniani, ambapo katika top 5 ya nchi zenye furaha ilishikwa na Finland, Norway, Denmark, Iceland na Uswisi huku Tanzania ikiwa moja kati ya nchi za mwisho kabisa kwa nchini zisizo na furaha.
Japokuwa inaelezwa kuna uwezekano nchi hizo, watu wake wana furaha kutokana na pato kubwa la taifa pamoja na msaada mkubwa wa kijamii kwenye nchi zao, inadaiwa kuwa watu wasio wazawa wa nchi hizo hawana furaha kama walivyo wazawa.
Siku hii ya Furaha duniani ilitengenezwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukuza ufahamu wa umuhimu wa mbinu ya umoja zaidi, usawa na ukuaji wa uchumi ulio sawa ambao utasaidia maendeleo endelevu, kumaliza umasikini, furaha na ustawi wa watu wote kwenye jamii.
Maneno ya Prof Tibaijuka baada ya Rugemalira kuendelea kusota Rumande