Kutoka nchini Ufaransa leo March 20, 2018 ni Rais Mstaafu wa nchi hiyo Nicolas Sarcozy anashikiliwa na polisi ili waweze kumfanyia mahojiano.
Inaelezwa kuwa Rais huyo Mstaafu anakabiliwa na tuhuma za makosa ambayo yaliyojitokeza katika fedha za kuendesha kampeni ya Uchaguzi Mkuu kipindi akigombea mwaka 2007.
Tuhuma hizo zinahusishwa na nyingine za kupokea pesa kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi katika kipindi cha uchaguzi huo ili kufanikisha ushindi wake. Sarcozy amekataa kuhusika na tuhuma hizo.
Hatimae upelelezi kesi ya Mhasibu TAKUKURU umekamilika