Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi ya India Sushma Swaraj ametangaza rasmi kuuawa kwa wafanyakazi 39 ambao walikuwa wanafanya shughuli za ujenzi kabla ya kutekwa na kuuawa na Kikundi cha Wanamgambo wa Kiislam nchini Iraq (IS).
Raia hao wa India walikuwa wametekwa tangu mwaka 2014, lakini serikali ilidai kuwa kuna uwezekano kuwa bado wako hai na juhudi za kuwapata ziliendelea hata baada ya kukuta watu 38 wamezikwa kwenye kaburi moja.
Waziri Swaraj ameeleza kuwa miili hiyo ilipimwa DNA na wakakuta inafanana kwa asilimia 70 na ya watu hao ambao walipotea kwa kutekwa mwaka 2014,
Mwaka 2014 serikali ya India ilitoa taarifa rasmi ya kuwashauri wananchi wake kutosafiri kwenda Iraq na hata ambao wako nchini Iraq waondoke nchini humo.
Mchungaji awalazimisha Waumini kubusu na kulamba viatu vyake