Leo March 20, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho March 21, 2018 atawaapisha Mabalozi Wateule wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli atamuapisha IGP-Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.
Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi Wateule hao itafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi.
Mchungaji awalazimisha Waumini kubusu na kulamba viatu vyake