Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amesema agizo la kila mkoa kuhakikisha unajenga viwanda vipya 100 kuanzia December 2017 hadi December 2018 limetekelezwa vizuri ambapo katika robo ya kwanza ya utekelezaji jumla ya viwanda 1285 sawa na asilimia 49.4 vimejengwa katika mikoa 26 Tanzania Bara
Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo December 2018, mikoa yote 26 ya Tanzania Bara inakuwa na viwanda vipya 2600 ili kufikia nchi ya uchumi wa kipato cha kati kupitia ujenzi wa viwanda ambapo hii leo Wakuu wa mikoa yote Tanzania Bara wanakutana hapa mjini Dodoma kupitia ajenda ya uchumi wa viwanda
Rais Magufuli kumuapisha IGP Mstaafu Mangu kuwa Balozi