Kufuatia operation ya kukamata wateja waliopata huduma ya umeme kinyume na taratibu mkoani Kagera inayoendeshwa na Afisa usalama na ukaguzi wa TANESCO mkoa humo Stephen Maganga kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo wamekamata zaidi ya wateja 13 na kuwaondolea huduma hiyo katika kata ya Kemondo wilaya ya Bukoba.
Wakiwa katika kata hiyo ya Kemondo wamefika kwa mteja mmoja Vedastina Josephat, ambapo baada ya kuelezwa kuwa anatakiwa kulipa faini kutoka na huduma aliyoipata, amesema kuwa hawezi kulipa faini hiyo badala yake italipwa na Yule aliyemuunganishia umeme.