Baada ya kuenea kwa taarifa mitandaoni kuwa mchezaji wa Singida United Danny Lyanga aliyejiunga na timu hiyo akitokea ya Oman kuwa amefungiwa na FIFA kutokana na kusaini Singida akiwa bado ni mchezaji wa Fanja FC.
Uzito wa taarifa hizo ulizidi kuenea baada ya mchezaji huyo kutoonekana akiitumikia Singida United katika michezo ya Ligi Kuu na watua kuanza kuamini kuwa inawezekana ikawa kweli kafungiwa, leo Singida United imetoa taarifa rasmi kuhusiana na taarifa hizo.
“Mchezaji wetu Daniel Lyanga hajatungiwa miezi sita kucheza soka, Klabu yetu ya Singida United ilifuata taratibu zote za usajili wa mchezaji Daniel Reuben Lyanga, usajili ulishirikisha pande zote mbili kati ya Fanja Fc na Singida United ikiwemo kulipa fidia za gharama wa mkataba wake uliokuwa umebakia kule Fanja FC”
“Taratibu ambazo zilipekea klabu yetu kupata release letter ya mchezaji na kuendelea na hatua za kiusajili. Kilichopo ni kwamba ITC ya Daniel Lyanga ilichelewa kuja kutokana na dirisha la usajili kufungwa, hivyo FIFA walituandikia barua sisi pamoja na TFF kwamba ITC ya Daniel Lyanga itakamilika hadi hapo dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa hapa Tanzania ( kunzia July/2018)”
“Hivyo basi ,Daniel Lyanga hajafungiwa na hivi tunategemea kumtumia kwenye michuano ambayo klabu yetu inakwenda kushiriki nje ya nchi. Maswala ya ITC kuchelewa,hayajaanza kwetu na hutokea katika soka”
“Tunaomba vyombo vya habari kutumia taarifa rasmi kutoka vyanzo rasmi kwa maslahi ya mpira wa miguu hapa nchini. Singida United milango yetu ipo wazi kutoa ushirikiano kwa jambo lolote ambalo chombo cha habari kinataka kujua, kufahamu au kushauri”
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry