Wanandoa na mastaa wa muziki kutokea Marekani Beyonce pamoja na mume wake Jay Z wamezua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana wakiwa Jamaica mtaa wa Trench Town katika boda boda (pikipiki) wakikatiza mitaa ya uswahilini huku watu wakiwashangaa.
Mtaa wa Trench Town ni maarafu sana nchini Jamaica kutokana na kuwa mkali wa Reggae marehemu Bob Marley aliishi mtaa huo na pia aliwahi kuuimba katika nyimbo zake mbalimbali.
Picha hizo zinazosambaa katika mitandao ya kijamii za wawili hao wamezipiga kwa lengo la kuitangaza ziara yao ya kimuziki ya OTR II ambayo inatarajiwa kuanza mwezi June 2018 na kumalizika October 2018.
Inasemekana pia Beyonce pamoja na Jay Z watashoot sehemu inayoitwa Tuff Gong ambapo ndipo ilipo nyumba na studio ya marehemu Bob Marley.
Maneno ya Jokate Mwegelo yaliowaacha mashabiki dilemma