Leo March 21, 2018 miongoni mwa stori ambayo ningependa ikufikie ni hii kuihusu Serikali ya Uingereza ambapo imetoa ruhusa kwa familia ya mtoto Alfie Dingley wa miaka 6 ambaye anaugua ugonjwa wa kifafa kutumia bangi kama dawa ya kifafa kwa mtoto huyo ili kuokoa maisha yake.
Wazazi wa mtoto huyo Drew Dingley na Hannah Deacon ambao wamekuwa wakiiomba serikali ya nchi hiyo iwaruhusu kutumia mafuta ya bangi kama tiba ya tatizo la kifafa linalomsumbua mtoto wao.
Wakiongea baada ya kukutana na Waziri Mkuu Theresa May wazazi hao wameeleza kuwa wameruhusiwa tiba hiyo kwaajili mtoto wao kwa makubaliano maalumu.
Matumizi ya bangi ni kinyume na sheria nchini Uingereza na hii ndio sababu ya wazazi hao kuomba ruhusa ya kuitumia kwa mtoto wao huyo ambaye huanguka hata zaidi ya mara mia katika kipindi cha mwezi, kwa kumpa matone matatu tu kwenye ulimi kila siku.
HUKUMU KESI YA DAWA ZA KULEVYA: Kilichompata Masogange siku ya hukumu