Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe leo March 22, 2018 ataongozana na viongozi wengine wakuu wa chama hicho kwenda kuripoti polisi baada ya kutakiwa kuripoti kituoni hapo.
Mbowe ameeleza kuwa watakaokwenda polisi ni pamoja na Katibu Mkuu Vincent Mashinji,, Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima J. Mdee.
Wengine ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, John W. Heche, Mbunge, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu Esther N. Matiko.
FULL INTERVIEW: Mtoto gumzo Anthony Petro kaongea tusiyoyajua.