Kuna taarifa ambazo ni adimu kuzisikia hasa zile zinazohusu mtu kukataa kazi hasa yenye mshahara mzuri sasa leo March 22, 2018 kuna hii kumhusu Mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 16 ambae amekataa uteuzi wa kuwa mkuu wa wilaya nchini Somalia katika wilaya ya Hirshabelle.
Feisal Abdullahi Omar aliteuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Somalia Mohamed Ali Adle ambapo amesema uteuzi huo ulikuja baada ya watu kumtembelea baba yake na kuwaomba kupendekeza mwakilishi katika ukoo wao.
”Nilipokuwa nikisubiri mkutano wa ukoo, nilipata barua ya uteuzi huo kutoka kwa waziri ambaye alimpatia baba yangu barua hiyo. Nilishangaa. “lakini nilikataa uteuzi huo kwa kusema kwamba asingeweza majukumu ya nafasi hiyo ya uongozi” -Feisal
Aliongeza kuwa kuna changamoto kubwa katika mkoa anaoishi kuhusiana na masuala ya usalama .
”Ninahofia usalama wangu mwenyewe, Siwezi kuchukua jukumu hilo kwa sababu hali ya usalama katika nchi hii sio nzuri “ -Feisal