Leo March 22, 2018 nakusogezea Utafiti uliofanywa na Watafiti wa Marekani ambapo wamegundua matatizo 10 mapya ya mtandao wa 4G ambayo yatasababisha ukosefu wa usalama, na kutoa wito kuwataka watu husika kufanya juhudi pamoja ili kutatua matatizo hayo.
LTE ni moja ya teknolojia za mtandao wa 4G. Watafiti wa Chuo Kikuu cha Purdue na Chuo Kikuu cha Iowa nchini Marekani wakitumia njia ya majaribio iitwayo “LTE inspector” wamegundua matatizo hayo.
Watafiti wamesema wadukuzi wanaweza kutumia matatizo hayo kudukua njia za kutuma na kupokea ishara, kutuma ujumbe feki kwa simu nyingi, kuzilazimisha simu kufanya kazi fulani mpaka betri inakwisha, kuzuia simu kuungana na mtandao mkuu, kuungana na mtandao mkuu bila idhini, na kuzifanya server zisifanye kazi.
Watafiti wamefanya majaribio ya matatizo 8 kati ya matatizo hayo 10, na kugundua kuwa ni vigumu kutatua matatizo hayo. Watu huenda wanatakiwa kurekebisha mtandao kamili wa 4G LTE ili kutatua matatizo hayo.