Upepo wa viongozi wakubwa wa serikali mbalimbali duniani kujiuzulu au kuvuliwa madaraka unaendelea, ambapo Rais mwingine amejiuzulu baada ya Rais waMyanmar Htin Kyaw kujiuzulu jana March 21, 2018.
Jana hiyo hiyo Rais wa Peru, Pedro Pablo Kuczynski pia ametangaza rasmi kujiuzulu kutoka kwenye kiti chake hicho cha urais ikiwa ni miezi 6 tu tangu aingie madarakani.
Rais Kuczynski tangu aingie madarakani amekuwa akikabiliwa na tuhuma za rushwa na kile kinachoitwa unyanyasaji wa kisiasa.
Rais huyu amejiuzulu siku moja kabla ya siku ambayo Bunge la nchi hiyo liliahidi kupiga kura ya kumuondoa madarakani.
Madaktari wa Apollo Hospital India wanaeleza Presha inavyosababisha Stroke ya Ubongo