Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2017 imegundua kuwa matukio ambayo yalisababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi duniani kote ambayo yanagharimu fedha nyingi.
Inaelezwa kuwa matukio hayo yamegharimu Dola za Marekani Bilioni 320 kwa mwaka 2017 pekee ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 768 na ripoti hii inaeleza hali hiyo kujirudia mwaka 2018 na kuharibu maisha ya watu.
Umoja wa Mataifa kwenye taarifa yake leo March 22, 2018 inaeleza kuwa miaka mitatu iliyopita imekuwa ndio miaka yenye joto kali zaidi kuwahi kutokea duniani jambo lililosababisha majanga kama Joto la Arctic na uhaba wa maji nchini Afrika Kusini.
Hatimaye Upelelezi kesi ya Viongozi wa Simba Aveva, Kaburu umekamilika