Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa March 22 2018 ilikuwa nchini Algeria kucheza mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Algeria, game hiyo Taifa Stars alicheza ugenini.
Taifa Stars inacheza dhidi ya Algeria ikiwa ni miaka mitatu imepita toka wakutane mara ya mwisho November 17 2015 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018, game ambayo ilichezwa Algeria katika uwanja wa Mustapha Tshacker na game ilimalizika kwa Tanzania kupoteza kwa magoli 7-0.
Kwa mara nyingine tena Taifa Stars anapoteza mchezo dhidi ya Algeria kwa magoli 4-1,magoli ya Algeria yalifungwa na Bounedjah dakika ya 12na 79, Shomari Kapombe akajifunga kwa kichwa dakika ya 44 na Medjani aliyefunga dakika ya 53 wakati goli pekee la Tanzania la kufutia machozi lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 12.
Mchezo wa leo kwa Taifa Stars ulilenga kucheza ili kupanda katika viwango vya FIFA endapo wangeshinda kutokana na Algeria wao wanashika nafasi ya 60 katika viwango vya FIFA na Tanzania wapo nafasi ya 146, hivyo baada ya kupoteza sasa wanarudi Tanzania nyumbani kucheza dhidi ya DRC Congo game nyingine ya kirafiki Congo wakiwa nafasi ya 39 katika viwango vya FIFA.
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry