Leo March 22, 2018 Kampuni ya Kitty Hawk inayomilikiwa na mwanzilishi wa kampuni ya Google Larry Page imetoa taarifa kuwa imefanya majaribio ya teksi mpya inayoruka.
Kampuni hiyo imesema kuanzia mwezi October 2017, kampuni hiyo ilianza kufanya majaribio ya teksi inayoruka iitwayo Cora nchini New Zealand. Teksi hiyo haitauzwa kwa wateja binafsi, bali itatumiwa kwa usafirishaji wa umma.
Teksi inafanana na ndege ndogo au ndege isiyokuwa na rubani. Ndege hiyo inaweza kwenda juu na kushuka chini moja kwa moja kama helikopta, kuruka kwenye barabara ya ndege kama ndege yenye mabawa, inaweza kuruka kwa kilomita 100 na kwa urefu wa mita 150 hadi 900 angani na kwa mwendo kasi wa kilomita 170 kwa saa.
Kampuni hiyo imesema kuna kompyuta tatu kwenye teksi hiyo, hata kompyuta moja ikiharibika, teksi hiyo bado inaweza kuruka. Parachuti pia imewekwa kwenye teksi ili kukabiliana na hali ya dharura. Teksi hiyo inaendeshwa na software na kudhibitiwa na binadamu, hivyo hata mtu asiyeweza kuendesha ndege anaweza kuendesha teski hiyo.