Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha taarifa kuhusu Serikali kutaka kufungia mitandao ya kijamii nchini kama ilivyokuwa ikisambaa katika mitandao na sehemu mbalimbali.
Gerson Msigwa kupitia ukurasa wake wa Twitter amewataka wananchi kupuuza barua iliyoonekana mitandaoni ikionesha imetolewa na ikulu ikiwaonya wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kwa faida ili kuleta maendeleo la sivyo Serikali itaifungia.
Nanukuu alichoandika Msigwa katika Twitter yake “Taarifa hii imetengenezwa na wahalifu wa mtandao. IPUUZWE”
Taarifa hii imetengenezwa na wahalifu wa mtandao. IPUUZWE. pic.twitter.com/frwWozW12U
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) March 24, 2018
ALICHOAGIZA RAIS MAGUFULI KWA WAZIRI MKUU WA ISRAEL NETANYAHU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA NA KUSIKILIZA