Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba leo March 26, 2018 ameonya kuhusu maandamano yanayopangwa kwani ndani yake watakuwepo watu ambao watafanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.
Waziri Mwigulu ameeleza kuwa lengo la serikali si kuminya uhuru wa maandamano kwani yapo kikatiba bali wapo watu ambao watatumia mwaya wa maandamano hayo kuvuruga amani ya nchi.
“Tunaangalia sura ambayo adui anaweza kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa ni vitu vyepesivyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya yanapojitokeza.” – Waziri Mwigulu
Waziri Mwigulu amezungumza hayo katika Harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri katika Usharika wa Masaka Dayosisi ya Pare, wilayani Same.
Hakimu amemuachia kwa dhamana Abdul Nondo