Katika kukabiliana na athari za kuongezeka kwa mwingiliano wa watu kutokana na mitandao ya kijamii inayosababisha kuongezeka kwa taarifa za uongo duniani, Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limeanzisha mpango maalumu.
BBC imeanzisha mchakato utakaohusisha waandishi wake wa habari kwenda shuleni na kufundisha wanafunzi kuhusu jinsi ya kutambua habari za uongo.
Mpango huo umeundwa ili kukabiliana na habari za uongo ambazo shirika hilo linasema kuwa zinatishia mijadala ya msingi kwenye jamii na kuaminiwa kwa weledi wa waandishi wa habari.
Maelezo zaidi juu ya mpango huo, ambao utahusisha hadi shule 1,000, unatarajiwa kuwekwa wazi katika mpango wa mwaka mzima wa shirika hilo siku ya Jumatano March 28, 2018.
“Wahubiri wawaeleze Watanzania tunapoteza Bilioni 500” – JPM