Bunge nchini Malaysia limependekeza sheria mpya ya kudhibiti ongezeko la kusambaa kwa habari za uongo nchini humo ambapo watakaokutwa na hatia ya makosa hayo watatumikia kifungo cha hadi miaka 10 jela.
Katika adhabu hiyo watuhumiwa watafungwa miaka hiyo jela au kulipa hadi Dola za Kimarekani 128,000 ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania milioni 307 kama faini.
Muswada huu umewakilishwa Bungeni jumatatu ya leo March 26, 2018 kipindi ambacho nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi wake mkuu.
Alichosema Diwani CHADEMA baada ya kupiga picha na RC Gambo