katika kuhakikisha jiji la DSM linapiga hatua katika utalii, Mameya wa jiji hilo wamefanya ziara katika Jiji Arusha kwa lengo la kujifunza na namna gani jiji la Arusha limeweza kupiga hatua katika sekta ya utalii pamoja na usafi wa mazingira hatua ambayo itawasaida kutekeleza mambo hayo katika jiji la DSM.
Akiongea na Mameya wenzake Meya wa Jiji la DSM Isaya Mwita amewataka viongozi hao kuacha kuangalia vyama walivyotoka na wafanye kazi kwa bidii ili kuwaleta wananchi maendeleo na mambo ya vyama wasubiri uchaguzi 2020.