Shirika la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wamesema uamuzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kumsimamisha masomo Mwenyekiti wa TSN Abdul Nondo kabla ya kumalizika kwa kesi inayomkabili mahakamani, ni sawa na kumhukumu kabla ya kesi hiyo kumalizika.
Akizungumza na waandishi wa habari Onesmo Olengurumwa ambae ni Mratibu THRDC amesema uamuzi wa UDSM unakwenda kinyume na haki za binadamu na Katiba ya nchi.
” Nondo hata kesi yake ukiangalia aliripoti kama mlalamikaji lakini kilichotokea ndiyo hicho sasa kabla ya ukweli haujajulikana chuo nao wanatoa uamuzi huo kwa kweli hawajamtendea haki mwanafunzi huyu,” -Olengurumwa
BREAKING: ”Siko vizuri Kiakili, Barua Nimeona kwenye Mitandao”- Nondo