Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Arusha imewafikisha mahakamani wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya jumla ya Dola za Kimarekani 35,500 sawa na Shilingi Milioni 85.
Wakili wa TAKUKURU Adam Kilongozi akiwasomea mashtaka hayo ameiambia mahakama hiyo kwamba watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo katika mageti ya Nahalu mkoani Mara na Lodware lililopo mkoani Arusha.
Watuhumiwa hao ni Joseph Mtwalo, John Mlambo Mwahu Yunusi, Mary Njau, pamoja na Catherine Edward.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Bernard Ngaga ameahirisha kesi hiyo hadi April 10 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kulipa bondi ya zaidi ya Shilingi milioni saba.
BREAKING: ‘Nondo hajakosea ndani ya Chuo’-Haki za Binadamu