Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kupoteza mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Algeria kwa magoli 4-1 nchni Algeria, leo uwanja wa Taifa walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Congo DRC.
Timu ya taifa ya Congo DRC iliyocheza na Taifa Stars ilikuja na wachezaji wengi wanaocheza nje ya bara la Afrika, huku kutoka ndani ya Afrika wakiwa wachezaji wawili pekee, ukilinganisha na Taifa Stars ambao ina mchezaji mmoja tu Mbwana Samatta ndio anacheza nje ya Afrika.
Congo DRC kuja na wachezaji ma-professional wengi katika kikosi chao hakuja saidia chochote na wamejikuta wakipoteza mchezo kwa magoli 2-0, magoli ya Taifa Stars yakifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 74 kabla ya Shiza Kichuya kuitumia vyema pasi ya Samatta dakika ya 85 na kufunga goli la pili.
Tanzania hadi sasa wapo nafasi ya 146 katika viwango vya soka vya FIFA vinavyotolewa kila mwezi wakati Congo DRC wao wapo nafasi ya 39 katika viwango vya soka vya FIFA na wakiwa nafasi ya tatu katika viwango vya soka kwa Afrika baada ya Tunisia na Senegal.
EXCLUSIVE: Kingine usichokifahamu kutoka kwa Victor Wanyama wa Tottenham