Baada ya timu ya taifa ya Argentina kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Italia na kupata ushindi wa 2-0 weekend katika uwanja wa Etihad jijini Manchester huku staa wao Lionel Messi akiwa benchi, leo wamecheza game yao ya pili ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Hispania katika jiji la Madrid nchini Hispania.
Argentina leo wamemkosa staa wao Lionel Messi kutokana na kusumbuliwa na misuli na wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 6-1, magoli ya Hispania yamefungwa na Diego Costa dakika ya 12, Isco aliyefunga hat-trick dakika ya 27, 52 na 75, Thiago dakika ya 55 na Iago Aspas dakika ya 73 wakati goli la kufutia machozi la Argentina likifungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 39.
Hat-trick ya Isco ndio inakuwa hat-trick yake ya kwanza akiichezea timu ya taifa ya Hispania ya wakubwa lakini jeraha la Lionel Messi limeanza kuleta presha kwa mashabiki wa timu yake ya FC Barcelona na kuanza kuhofia kama atapatikana katika mchezo dhidi ya Sevilla lakini wakiiwazia pia game yao ya robo fainali ya UEFA dhidi ya Roma itakayochezwa wiki ijayo Lionel Messi atakuwa fiti?
VideoMAGOLI: Samatta na Kichuya walivyowaua Congo leo March 27, Full Time 2-0