Leo March 28, 2018 Hatimaye upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha wa USD 375,418 inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Baada ya kueleza hayo, Swai aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Baada ya kueleza, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi April 11, 2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Mbali ya Malinzi, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga.
Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza June 29,2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha USD 375,418. 7