Moja kati ya habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii leo ni kuhusiana na winga wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea club ya Simba SC Shiza Ramadhani Kichuya kudaiwa kuhitajika na club ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Baada ya kiwango kizuri alichokionesha katika mchezo wa timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Congo DRC uliyomalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa magoli 2-0, zimeenea tetesi katika mitandao ya kijamii kuwa TP Mazembe imeanza kumfuatilia Shiza Kichuya.
Game ya Taifa Stars dhidi ya Congo ilimalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa magoli 2-0, huku Shiza Kichuya akihusika moja kwa moja katika upatikanaji wa magoli yote mawili kwani alitoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na Samatta na akafunga goli la pili.
Kama tetesi hizo zitakuwa kweli na Shiza Kichuya kupata nafasi ya kucheza TP Mazembe atakuwa anafuata nyayo za Mbwana Samatta aliyewahi kuichezea TP Mazembe kwa miaka mitano kabla ya kwenda kujiunga na Club ya KRC Genk ya Ubelgiji mwaka 2016.
VideoMAGOLI: Samatta na Kichuya walivyowaua Congo leo March 27, Full Time 2-0