Watu watano wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea leo March 29, 2018 jioni katika maeneo ya Kasharazi ulipo Mlima wa K9 {K’nine} mkoani Kagera baada ya gari lililokuwa likisafirisha wakimbizi kutoka Kigoma kuelekea Burundi kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu hao.
Kamanda wa Polisi Kagera Augustine Ollom amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema yapo magari mawili yaliyokuwa yakiwasafirisha wakimbizi kurudi nchini kwao, yalipata ajali baada ya Bus moja kugonga lingine na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi.
Ameyataja magari hayo kuwa lipo gari lenye namba za usajili T331 DFV aina ya YUTONG liligonga Bus T765 DLD aina ya TATA ambapo lilipoteza uelekeo na kumgonga mwendesha Baiskeli na akafariki palepale, kati ya hao wengine waliopoteza maisha ambao majina yao bado hayajatambulika wapo wakiume wawili na wa kike wawili.
BREAKING: Mbowe, Viongozi Watano CHADEMA wapewa masharti ya dhamana