Mahakama Kuu ya Kenya imewatoza faini ya Ksh. 200,000 (TSH. MILIONI 4.4) Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Gordon Kihalangwa na IGP Joseph Boinnet kwa kutofika mahakamani kueleza sababu ya kumzuia Miguna kuingia nchini humo.
Jaji George Odunga aliwaamuru maafisa hao waandamizi wa serikali kufika Mahakamani siku ya Jumatano, kwa ajili ya kuhukumiwa, baada ya kutiwa hatiani kwa kudharau Mahakama baada ya kukaidi amri ya kumuachia mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna.
Jaji ameagiza pesa hizo zikatwe kwenye mishahara yao.