Leo March 30, 2018 askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Evaristo Marc Chengula, amewataka waumini wa kanisa hilo nchini Tanzania kuchagua viongozi sahihi na watakaokidhi mahitaji yao badala ya kufanya makosa kwa kuchagua viongozi wasiofaa na kuanza kulalamika baada ya uchaguzi.
Askofu Chengula ametoa ujumbe huo katika mahubiri aliyotoa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu inayofanyika katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Parokia ya Mtakifu Francisco wa Asizi, Mwanjelwa mkoani Mbeya.
Amesema imekuwa ni kawaida kwa maaskofu na wadau wengine kuanza kukosoa viongozi baada ya uchaguzi, jambo ambalo halina faida, hivyo wao kama maaskofu mwaka huu wameamua kuwataka waumini wao kuwapima kwa umakini watu wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.
“Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote, tukipata viongozi wazuri tutafurahi wote, kila mmoja aone kiu ya Tanzania hii kuwa nchi ya upendo,” -Askofu Chengula
BREAKING: “Silaha iliyomuua AKWILINA haijajulikana bado” -Kamanda Mambosasa