Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa leo April 02, 2018, amewasha Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018, ambapo Kitaifa umewashiwa mkoa wa Geita, pamoja na uwashaji wa Mwenge Waziri Mkuu wakati akiongea na wananchi wa Geita ametaja Mikoa inayoongoza kwa utoro mashuleni kwa Sekondari na shule za Msingi na mkoa wa Geita unashika nafasi ya pili kwa utoro mashuleni.