Katika kisa cha kusikitisha huko nchini India kijana mmoja ambaye ni wa jamii ya Dalit amepigwa hadi kufa na wanaume watatu kutokana na kijana huyo kumiliki na kuendesha farasi.
Inaelezwa kuwa marehemu huyo ambaye anatokea kwenye jamii ya tabaka la chini alipigwa hadi kuuawa na wanaume hao ambao wao wanadaiwa kutokea tabaka la juu kiuchumi kwa madai kwamba kijana huyo hana haki ya kumiliki farasi.
Katika jamii za India kama jamii nyingine nyingi duniani, familia zinazomiliki na kuendesha farasi zinaaminika kuwa familia tajiri, hivyo ni nadra kuona familia maskini wanamiliki farasi.
Polisi katika Jimbo la Gujara wamethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa tayari wamewakamata wanaume hao ili kuwahoji, huku baba mzazi wa marehemu akieleza kuwa mwanaye huyo alikuwa ameonywa asimuendeshe farasi huyo.
Video iliyonasa Mbowe na Viongozi CHADEMA wakifikishwa Mahakamani