Inawezekana umewahi kusikia vituko vya tumbili au nyani kuiba chakula au hata kumpora mtu chakula ambacho amekishika mkononi na mengineyo mengi.
Hatahivyo tukio la ajabu limetokea huko nchini India baada ya tumbili kuingia ndani ya nyumba na kuiba mtoto wa kiume kisha kukimbia naye huku mama mzazi akijaribu kumuokoa mwanaye bila mafanikio.
Tukio hilo limetokea katika Jimbo la Orissa lililopo Mashariki mwa nchi hiyo. Inaelezwa kuwa mwili wa mtoto huyo siku moja baada ya tukio hilo ulikutwa kwenye kisima ambacho kiko nyuma ya nyumba hiyo baada ya jitihada kubwa zilizofanywa na wanafamilia kumtafuta.
Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo, huu wakiendelea kumsaka tumbili huyo.
Video iliyonasa Mbowe na Viongozi CHADEMA wakifikishwa Mahakamani