Mbunge wa Uingereza Stella Creasy hivi karibuni amezindua kampeni ambayo inalenga kuwapa wanawake ushauri wa jinsi ya kukabiliana na pengo la malipo kijinsia.
Hii imetokea ikiwa ni siku chache tu kabla ya kampuni zote za nchini huko kuwasilisha ripoti ya jinsi wanavyowalipa wafanyakazi wao kulingana na jinsia zao.
Kampeni hiyo inayojulikana kama #PayMeToo ambayo imezinduliwa ikiwa na tovuti yake na akaunti zake za mitandano ya kijamii, itawatia moyo wanawake kufanya utafiti kama wanalipwa sawa na wanaume ambao wanafanya kazi sawa na kufungua mashtaka kama hawalipwi sawa.
LIVE: JPM Kwenye uzinduzi wa kituo cha kufua umeme Kinyerezi 2