Golikipa wa Manchester United David de Gea baada ya kuripotiwa kwa muda mrefu kuwa anataka kuondoka na kurudi Hispania, leo zimeripotiwa taarifa mpya kuhusiana na mpango wa golikipa huyo ambaye ameitumikia Man United toka 2011.
Leo mtandao wa dailymail umeripoti kuwa David de Gea ambaye anamaliza mkataba wake na Man United mwaka 2019, anajiandaa kusaini mktaba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia Man United, mkataba ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa pound 350000 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 1.1.
David de Gea aliripotiwa kutaka kuondoka Man United mwaka 2015 kwenda kujiunga na Real Madrid lakini licha ya vilabu na yeye kukubaliana kila kitu ila kuchelewa kwa document ndio kukamfanya ashindwe kujiunga na Real Madrid lakini bado anahusishwa nayo licha ya kuwa ana mkataba na Man United hadi 2019.
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL