Viongozi saba wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe leo April 3, 2018 wamekamilisha masharti ya dhamana.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imejiridhisha na nyaraka walizoziwasilisha wadhamini kwa ajili ya dhamana ya washtakiwa hao na imewakubalia kuwadhamini huku ikiwapa maelekezo kuhakikisha kuwa wanapatikana mahakamani kila wanapohitajika.
Masharti ya dhamana yao ni kusaini bondi ya Milioni 20 kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka ofisi za Serikali za mitaa au vijiji na kuripoti kituo kikuu cha Polisi kila Alhamisi.
Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, manaibu katibu wakuu John Mnyika (ara, Salum Mwalimu, Zanzibar, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa KaweHalima Mdee na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho, Ester Matiko wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine ikiwamo kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.