Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imewaachia huru kwa dhamana, viongozi saba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) badaada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa yakiwemo ya Uchochezi wa Uasi na kufanya mkusanyiko isivyo halali.
Washtakiwa hao ni Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika,Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko na Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Mbowe na Viongozi CHADEMA walivyofikishwa Mahakamani