Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amethibitisha kuwa kikosi chake kitamkosa Sergio Aguero katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Liverpool kutokana na kuwa majeruhi.
Sergio Aguero amekuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa sasa toka aumie goti mwanzoni mwa mwezi uliyoisha wakiwa mazoezini na hajasafiri na timu kuelekea mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Guardiola ameeleza kuwa Aguero atapatika katika mchezo wa Ligi dhidi ya Manchester United siku ya Jumamosi “tumekuja hapa kucheza hii game japokuwa tunajua mashabiki wa Liverpool watawapa presha sana wachezaji ila hivyo ndivyo ilivyo”
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL