Leo April 3, 2018 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya DSM, linamshikilia Mbunge wa Tarime Vijini, John Heche (CHADEMA), kwa tuhuma za kushindwa kuripoti polisi kama alivyotakiwa jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu DSM, Lazaro Mambosasa amethibitisha kushikiliwa kwa mbunge huyo.
“Ni kama alivyoshikiliwa mwenzake Mdee naye hakuripoti, walikuja wakatakiwa kurudi wote wao hawakurudi, hakuna kosa jipya kosa lake ni kutorudi hadi wenzake wanapelekwa mahakamani,” -Mambosasa.