Shirkisho la soka barani Afrika CAF leo April 3 2018 kutoka makao makuu ya shirikisho hilo Cairo Misri, limetoa taarifa rasmi kwa vilabu vya Yanga SC ya Tanzania na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia kuwa kuna wachezaji hawatoruhusiwa kuwatumia.
CAF wametuma taarifa inayowazuia Yanga kuwatumia wachezaji wake wanne ambao ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Said Juma huku Dicha wakikatazwa kuwatumia wachezaji wake wawili ambao ni Teklu Tafese na Eshetu Mena katika mchezo dhidi yao.
Yanga na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia watacheza mchezo wao wa kwanza wa mtoano wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho Afrika jijini Dar es Salaam kati ya April 6-8, hivyo wachezaji hao hawaruhusiwi kutumika kutokana na kutumikia adhabu ya kadi za njano.
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL