Kufuatia ajali ya magari yaliyokuwa yakisafirisha wakimbizi kutoka Kigoma kuelekea nchini Burundi iliyotokea March 29, 2018 Kagera katika wilaya ya Ngara na kusababisha vifo vya watu nane wakiwemo wakimbizi sita, muendesha baiskeli na mfanyakazi wa Shirika la IOM {International Organisation for Migration}, wakimbizi hao wamezikwa katika wilaya Ngara na hao wawili kuzikwa na ndugu zao.
Akiongea katika kuaga miili hiyo Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, amesema wakimbizi hao waliamua kwa hiari yao kurudi nchini kwao baada ya kupakimbia kwa zaidi ya miaka minne wakiamini sasa kuna amani na kutumia nafasi hiyo kuongeza kuwa Tanzania tuendelee kudumisha amani na kuwakemea wale wanaofikiri kwamba kwenye vurugu watapata manufaa.