Leo April 4, 2018 stori ninayokusogezea ni kumhusu Prince Philip mwenye umri wa miaka 96 na ambae ni mume wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza, amelazwa katika hospitali London.
Prince Philip anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kiuno ambapo amekuwa na matatizo kwa muda mrefu.
Ujumbe kutoka Buckingham Palace umesema “Mfalme Philip alilazwa katika hospitali ya King Edward V11 Jumanne April 3 ambapo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kiuno chake hapo Jumatano April 4,”