Serikali ya Marekani imetoa magari 3 aina ya Toyota Land Cruiser kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ili kukabiliana na Ujangili na biashara ya usafirishaji wanyamapori.
Akikabidhi magari hayo, Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk.Inmi Patterson amesema magari hayo yatasaidia kuongeza uwezo wa askari katika kufanya doria za kupambana na ujangili.
“Kwa ushirikiano wa dhati kati ya serikali, raia wake, wabia wa maendeleo, asasi za kiraia na sekta binafsi tunaweza kulikabili na kulitokomeza janga hili la ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori,” -Dk.Patterson
Pia amesema serikali ya Marekani ni mbia mwenye fahari katika jitihada za Tanzania za kukabiliana na ujangili, ambapo imekuwa ikitoa mafunzo, vifaa na kufadhili shughuli za kujenga uwezo kwa askari.
Naye Mwenyekiti wa TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko amesema kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani utasaidia kupambana na ujangili.
“Sio kila siku tunasikiliza jambo moja, hawa wametusumbua” –Dr Tulia