Baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Paul Kisabo kutoa taarifa aPRIL 4 2018 kwamba Mwenyekiti wa mtandao huo Abdul Nondo ameitwa Ofisi za Idara ya uhamiaji ili kuhojiwa kuhusiana na uraia wake, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika yafuatayo.
Zitto kupitia akaunti zake za Twitter na Facebook ameandika jumbe ambazo zimeashiria kulaani kitendo hicho cha Abdul Nondo kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji, huku akimtaja babu yake Nondo kuwa Marehemu Mzee Omar Mitumba ambaye anadai ni mzaliwa wa Kigoma Ujiji.
Nondo ameagizwa kupeleka kwenye idara hiyo April 20, 2018 vyeti vya kuzaliwa, ikiwa ni cha kwake, vya wazazi wake pamoja na vyeti vya babu na bibi zake wa pande zote mbili ambapo Zitto Kabwe pia alisema ataambatana nae.
“Nitampeleka Abdul Nondo uhamiaji tarehe 20 April kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma mjini (Jimbo analotoka Abdul na Wazazi wake na Mababu zake) Wananchi wa Kigoma Mjini waliopo Dar watakaotaka kunisindikiza Mbunge wao kumpeleka Abdul huko sitawazuia, Anyways Mwami lazima asindikizwe” – aliandika Zitto Kabwe
Zitto alimalizia kwa kusema “Siku hiyo uhamiaji watatuambia kama Kigoma sio Tanzania ili tuwaombe wasio wa Kigoma warudi Tanzania maana haiwezekani waliowengi pasiwe kwao na wachache ndio iwe kwao”
Alichozungumza Balozi wa Marekani baada kutoa msaada wa magari