Baada ya club ya Azam FC kuondolewa katika michuano ya Kombe la FA katika hatua ya robo fainali na Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penati 9-8, zilianza kuenea tetesi katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa Azam FC wameamua kumuondoa CEO wao Abdul Mohammed kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu.
Taarifa zilizokuwa zinaenea zinaeleza kuwa Azam FC wameamua kumuondoa CEO wao kutokana na timu yao kutolewa Kombe la FA huku Ligi Kuu ikidaiwa kuwa haitakuwa na nafasi ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu, kwani wamiliki wa Azam FC wasingependa kuona kwa mara ya pili mfululizo club yao inashindwa kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani.
Hizo zilikuwa tetesi tu ila AyoTV leo ilimpata Afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga na kumuomba azungumzie ukweli kuhusiana na tetesi hizo, Ni kweli Abdul Mohamed kaondolewa katika timu “Hadi sasa sijapewa taarifa zozote na uongozi kuhusiana na Abdul Mohamed, Mohamed yupo ofisini kwake anaendelea na kazi kama kawaida”
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL