Taarifa kutoka mkoani Tabora asubuhi hii ya leo April 6, 2018 ni kutokea kwa ajali Igunga mkoani Tabora ambapo basi la City Boys lililokuwa likitokea Karagwe kwenda DSM kugongana uso na fuso na inasemekana kuna watu wamefariki ila bado idadi yao haijathibitishwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa alipopigiwa simu kuthibitisha ajali na kuweza kufahamu idadi ya vifo simu yake ilipokelewa na RCO nakusema RPC yupo anahangaikia majeruhi atatoa taarifa kamili akimaliza.