Kutoka nchini Rwanda, mwanafunzi wa Udaktari katika chuko kikuu kimoja mjini Kigali Joel Gasana ameunda programu ya simu kwa ajili ya wagonjwa wa Ukimwi.
Gasana ametengeneza programu hiyo ili iwasaidie wagonjwa wa Ukimwi kufuatilia matibabu yao.
Utafiti kutoka nchini humo unaonyesha kwamba asilimia 27 ya wenye maambukizi ya Ukimwi, hawazingatii matibabu yao kama inavyotakiwa hivyo programu hiyo itakuwa mahususi kwaajili ya kuwakumbusha.
Kutengenezwa kwa programu hii kumegundulika pale wanasayansi 16 kutoka nchi mbalimbali Afrika waliposhiriki katika shindano huko Rwanda la kutafuta ufumbuzi kwa changamoto kubwa zinazozikumba jamii za Afrika.
Idadi ya Watanzania wanaopata Saratani kila mwaka