Leo April 6, 2018 Mzee Jumanne Ngoma ambae ndiye Mgunduzi wa madini ya Tanzanite, amezungumza mbela ya Rais John Magufuli na kusema Serikali inautambua mchango wake na kumpa Shilingi Milioni 100.
Mzee Ngoma amezungumza wakati wa uzinduzi wa ukuta ulliojengwa na serikali kuzunguka mgodi wa Tanzanite, Magufuli amesema atampa barua Mzee Ngoma ya kutambua mchango wake katika ugunduzi wa madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee.
Mzee Ngoma alimshukuru Rais Magufuli na kusema alibaini kuwa kiongozi huyo amechaguliwa na MUNGU tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2015.
“Ninakushukuru sana Rais, kwa heshima hii na kunitambua mimi kama mgunduzi wa madini, ni heshima kubwa kwangu na niseme kuwa wewe umechaguliwa na Mungu, Wananchi wa Mirerani huyu ni Rais wa wanyonge, mimi nisingejulikana leo hii, hii ni furaha kubwa.” -Mzee Ngoma
“Natoa pongezi zangu kwako kwa kunitambua kunitambua, Watu wote hawa wanashiba kwa ajili ya jasho la mkono wangu” -Mzee Ngoma
Anaedai kugundua Tanzanite aomba kukutana na JPM
FULL STORY: Rais Magufuli kutoa MILIONI 100, mengine aliyozungumza Mirerani