Utafiti unaonesha kuwa watu bilioni 2.5 duniani wanahitaji miwani lakini wanashindwa kuzinunua kutokana na gharama zake kuwa juu sana. Inaelezwa kuwa takriban asilimia 80 ya watu hawa wanapatikana kwenye nchi 20 zinazoendelea hasa Afrika na Asia.
Taasisi ya ODI Think tank inatahadharisha kuwa tatizo la uoni hafifu halipewi kipaumbele katika bajeti ya misaada inatolewa kwa dharura, ukilinganisha na matatizo mwengine ya afya kwenye nchi mbalimbali duniani.
Inaripotiwa kuwa uonaji hafifu katika nchi maskini, ni kikwazo cha elimu na ajira na husababisha familia kuwa maskini.
Idadi ya Watanzania wanaopata Saratani kila mwaka