Shirikisho la soka Tanzania TFF March 15 lilitangaza adhabu ya kumfungia maisha kujihusisha na soka makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu, moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi na kushusha hadhi ya TFF.
Baada ya kutangazwa kushindwa rufaa leo Mwanaseheria wa Wambura ambaye anajulikana kama Emmanuel Muga ameongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa walijua kuwa Wambura lazima afungiwe kwa sababu kamati hii iliundwa kwa ajili yake.
Makamu wa Rais wa TFF hatutamuona tena katika soka